MTEULE THE BEST
Aliyeteuliwa na Rais Donald Trump kuwa mkurugenzi mpya wa shirika la kijajusi la Marekani la FBI, Christopher Wray, ameahidi kufuata sheria bila kugemea upande wowote.
Wakati akihojiwa na wajumbe wa kamati ya senati ya sheria, bwana Wray amesema hafikirii kwamba uchunguzi wa tuhuma ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 kwamba una lengo la kutafutana kisiasa kama inavyodaiwa na Rais Trump.
Bwana Wray amesema katu hatoruhusu kazi ya FBI kuendeshwa na kitu chochote kile zaidi ya ukweli na sheria.
Uwezo wa Wray wa kusimama bila kuegemea upande wa Rais ulichukua nafasi kubwa ya kamati hiyo.
Mkurugenzi aliyepita wa shirika hilo, James Comey, alifutwa kazi na Trump kutokana na uchunguzi wa Urusi.
Christopher Wray alifanya kazi miaka minne katika wizara ya sheria chin
Maoni