MTEULE THE BEST
Mtoto wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump amevishambulia vyombo vya habari kufuatia madai ya mkutano na wakili mrusi ambaye alisema kuwa alikuwa na habari za kumchafulia jina Hillary Clinton.
Donald Trump Jr amekana kutoa habari za kukanganya kuhusu mkutano huo wa mwaka uliopita.
Pia amesema kuwa lilikuwa jambo la kawaida kupata taarifa kuhusu wagombea pinzani.
Maafisa nchini Marekani wanachunguza madai yanayohusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Mkwe wa Trump Jared Kushner na aliyekuwa mkuu wa kampeni Paul J Manafort, walikuwa pia katika mkutano huo na Natalia Veselnitskaya.
Trump Jr anasisitiza kuwa wakili huyo hakutoa taarifa muhimu kumhusu Bi Clinton, ambaye alikuwa mshindani wa babake katika kiti cha urais.
Mkutano huo ulifanyika tarehe 9 mwezi Juni mwaka 2016 katika jengo la Trump Tower, wiki mbili baada ya Donald Trump kupata uteuzi wa Republican.
Unaaminiwa kuwa mkutano wa kwanza wa siri kati ya raia wa Urusi na watu waliokuwa karibu na Bwana Trump.
Maoni