MTEULETHEBEST
Raisi wa zamani wa Brazili, Luiz Ignacio Lula da Silva, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa unusu jela miongoni mwa kesi tano za ulaji rushwa zinazomkabili.
Lula amechomoza kutoka katika umaskini wa kifamilia enzi za utoto wake na kuwa mmoja wa marais maarufu zaidi wa Brazil.
Kiongozi wa zamani wa chama cha muungano alijizolea pongezi kutoka katika jamii ya kimataifa kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kupunguza uhaba wa kina wa Brazil.
Lakini sasa mambo yamegeuka na kukutwa na hatia ya kukubali hongo ya zaidi ya dola milioni moja za malipo ya ghorofa ya mapumziko kwa ajili ya ukarabati wake kwa kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, iitwayo kwa kifupi OAS.
Hukumu hii inakuja wakati ambapo mtawala Lula akiwa ametoa msimamo mkali kwamba ana mpango wa kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais mwakani .
Kufuatia hukumu hiyo, rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo, huku mawakili wanaomtetea wameapa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Maoni