Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

KRISTO NA KAZI YAKE

MTEULE THE BEST  TUMSIFU YESU KRISTO WAPEDWA KATIKA KRISTO!!! MADA YA LEO : KRISTO NA KAZI YAKE SOMO:WAKOLOSAI 1:15-23   Kristo ni mfano wa MUNGU asiyeonekana; ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Maana kwake viumbe vyote viliumbwa kila kitu duniani na mbinguni vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: wenye enzi, watawala,wakuu na wenye nguvu  Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake. Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote ; vyote uendelea kuwako kwa uwezo wake. Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye nichanzo cha uhai yaani huo mwili. Yeye ndiyo mwanzo , mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka wafu ili awe na nasfi ya kwanza katika vitu vyote. Maana MUNGU aliupenda utimilifu wake woteuwe ndani yake. Kwake vitu vyote vilipatanishwa na MUNGU: na kwa damu yake msalabani akafanya amanina vitu vyote duniani na mbinguni. Hapo kwanza nyinyi pia mlikuwa mbali  na MUNGU na mlikuwa adui zake kwa sababu ya fikra zenu na matendo yenu maovu. L...

Novak Djokovic abanduliwa

MTEULE THE BEST   Novak Djokovic amebanduliwa katika mashindano ya Wimbledon baada kushindwa na raia wa Marekani Sam Querrey na hivyobasi kusitisha matumaini ya mchezaji huyo aliye nambari moja duniani kushinda taji la mwaka la Grand Slam. Querrey,aliyeorodheshwa nambari 28,alishinda kwa seti 7-6 {8-6} 6-1 3-6 7-6 {7-5} katika raundi ya tatu baada ya mvua kusitisha mchezo kwa mda. Ni mara ya kwanza kwa raia huyo wa Serbia kushindwa katika shindano kubwa tangu 2015 wakati wa fainali za French Open.   Djokovic Djokovic alikuwa na matumaini ya kushinda taji lake la tatu mfululizo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 tayari ameshinda mataji ya Australia na Ufaransa mwaka 2015.

Apple kununua Tidal ya Jay Z

MTEULE THE BEST   Kampuni ya Apple inadaiwa kutaka kuchukua umiliki wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja ya mwanamuziki Jay Z Tidal. Kampuni hiyo imeripotiwa kwamba inaangazia wazo la kuinunua huduma hiyo kutokana na ushirikiano wake na wanamuzika bingwa kama vile Kanye West na Madonna. Duru zimearifu jarida la Wall Street kwamba mazungumzo yameanza na huenda yakasababisha kupatikana kwa makubaliano. Msemaji wa Tidal amekana kwamba imefanya mazungumzo na Apple. Jay Z alizindua huduma hiyo mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kama mpinzani wa Spotify.   Jay Z Kampuni ya kiteknolojia ya Sweden, Aspiro ambayo ilikuwa ikiimiliki Tidal,ilinunuliwa na mwanamuziki huyo wa mtindo wa Rap kwa takriban dola milioni 56. Jay Z aliandamana na Kanye West. Alicia ...

Manchester United yamsajili Mkhitaryan

MTEULE THE BEST   Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan amesajiliwa na klabu ya Manchester United ,kulingana na klabu hiyo ya Ujerumani. Afisa mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema kuwa wamekubali kumuuza mchezaji huyo kwa United ili kumzuia nahodha huyo wa Armenia kuwa ajenti huru mwishoni mwa msimu ujao. ''Iwapo tungekataa mchezaji huyo angekuwa huru mwaka 2017'' ,Watzke aliambia mtandao wa Dortmund. United tayari imewasajili wachezaji wawili msimu huu akiwemo beki Eric Baily na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic. Mkhitayran alijiunga na Dortmund 2013 kutoka klabu ya Ukrain Shakhtar Donetsk kwa pauni milioni 23.  

Kikosi cha Kenya cha Olimpiki chatajwa

MTEULE THE BEST   Kamati ya olimpiki nchini Kenya, Nock, na shirikisho la riadha nchini Kenya, AK, zimetaja timu itakayoiwakilisha Kenya mjini Rio, nchini Brazil Agosti mwaka huu. Ingawa wanariadha wawili wa kwanza katika kila kitengo walijanyakulia tiketi, Kikosi cha Kenya pia kimeangazia masuala mengine kama vile fomu ya wanariadha, matokeo yao katika mbio za riadha duniani yakiwemo mashindano ya hivi karibuni ya riadha nchini Afrika Kusini. Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Olimpiki katika mbio za mita mia nane, David Rudisha, amepewa fursa nyingine ya kushiriki katika Olimpiki licha ya kubwagwa na Alfred Kipketer.   Yego Licha ya kujiondoa kutoka mbio za mita elfu kumi, bingwa wa Dunia, Geodfrey Kamworor ni miongoni mwa wanariadha watakaowania m...

Taliban laitaka Marekani kuondoka Afghanistan

MTEULE THE BEST   Kiongozi wa kundi la wapiganaji la Taliban amezungumza kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake mwezi mei, ambapo ameitaka Marekani kuondoka Afghanistan. Maulawi Haibatullah Akhundzada amesema uwepo wa Marekani na washirika wake nchini Afghanistan hautaathiri juhudi za makundi ya kijihadi.   Wapiganaji wa Taliban Amesema kuwa Taliban haitaki kuwa na ukiritimba wa mamlaka, japo akasisitiza kwamba ni Lazima serikali ya Afghanistan ikatize uhusiano wake na Marekani, kama hatua ya kwanza ya mchakato wa amani katika misingi ya sheria za kiislamu.  

Jeshi la Israel lashambulia Gaza

MTEULE THE BEST Ndege za kivita za Israeli zimetekeleza msururu wa mashambulzi ya asubuhi mapema huko Gaza. Jeshi la Israeli linasema limeshambulia maeneo manne yanayohusishwa na wapiganaji wa Hamas ambao wanadhibiti eneo hilo. Kulingana na taarifa kutoka kwa vyanzo nchini Palestina, watu wawili wameuawa.   Awali kombora lililofytuliwa kutoka Gaza liligonga jengo la shule ya chekechea japo halikuwa na watu.