KRISTO NA KAZI YAKE

MTEULE THE BEST

 TUMSIFU YESU KRISTO WAPEDWA KATIKA KRISTO!!!

MADA YA LEO : KRISTO NA KAZI YAKE

SOMO:WAKOLOSAI 1:15-23


 

Kristo ni mfano wa MUNGU asiyeonekana; ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

Maana kwake viumbe vyote viliumbwa kila kitu duniani na mbinguni vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: wenye enzi, watawala,wakuu na wenye nguvu  Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake.

Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote ; vyote uendelea kuwako kwa uwezo wake.

Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye nichanzo cha uhai yaani huo mwili.

Yeye ndiyo mwanzo , mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka wafu ili awe na nasfi ya kwanza katika vitu vyote.

Maana MUNGU aliupenda utimilifu wake woteuwe ndani yake.

Kwake vitu vyote vilipatanishwa na MUNGU: na kwa damu yake msalabani akafanya amanina vitu vyote duniani na mbinguni.

Hapo kwanza nyinyi pia mlikuwa mbali  na MUNGU na mlikuwa adui zake kwa sababu ya fikra zenu na matendo yenu maovu.

Lakini sasa, kwa kifo cha mwanae aliyeishi hapa duniani , MUNGU amewapatanisha naye, kusudi awaweke mbele yake mkiwa watakatifu , safi na bila lawama  

Mnapashwa lakini kuendelea na msingi imara katika imani  wala msikubali kutikishwa kutoka katika tumaini lile mlilopata wakati mlipo sikia injili  mimi PAULO nimekuwa mtumishi  wa hiyo injili ambayo imekwishaubiliwa na kila mtu duniani 

NENO LA BWANA............

Tumuombe Mungu atuongoze katika njia ya kweli na haki daima na milele

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU