FEDHA HULETA MATATIZO

MTEULE THE BEST

TUMSIFU YESU KRISTO WAPENDWA KATIKA BWANA

MADA YA LEO: FEDHA HULETA MATATIZO

SOMO  SIRA 31:1-11


Kukosa usingizi juu ya mali humdhoofisha mtu; kuhangaahika juu yake huondoa usingizi.

Mahangahiko ya usiku kucha hufukuza usingizi; ni kama ugojwa mkali, huondoa usingizi kabisa.

Tajiri hutoa jasho na kuchuma mali nyingi, kisha huketi chini na kuponda maisha

Masikini naye hutoa jasho na mali yake hupungua ,kisha huketi chini na hana chochote

Apendaye dhahabu hataoneka hana hatia, na atafutaye sana fedha atapotoshwa nayo.

Wengi wameangamia kwa sababu ya mali, na maangamizi hayo yamewavamia ana kwa ana.

Mali ni mtego kwa wanaovutwa nazo, na kila mpumbavu atanaswa nazo.

Heri mtu aliye tajiri bila lawama, mtu ambaye hakimbilii utajiri.

Ni nani huyo tumpe hongera?  Maana amefanya maajabu kati ya watu .

Nani aliyepata kujaribiwa na mali akaonekana bila hatia?  Mtu kama huyo anayo haki kujivuna!  Nani aliyepata nafasi ya kutenda dhambi asitende?  Nani aliyepata nafasi ya kufanya maovu asifanye?

Mtu kama huyo mali yake itadumu, na jumuiya itautambua ukarimu wake.

NENO LA BWANA!!!


LEO tumepata nafasi yakujua apendaye Mungu

Mali inadumu kwa mapenzi yake Mungu yakitimizwa halleluya!!!!!!

BWANA NI MWEMA NA VITU VYA NI VYEMA 

               AMINA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU