Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Colonel Mustafa -Dodoma Singida Video yafungiwa kenya

MTEULE THE BEST DODOMA SINGIDA KENYA MAARUFUKU KWENYE TV

GAB0N:Jean Ping, ametaka watu wasishirikiane na Ali Bongo

MTEULE THE BEST Image copyright GETTY IMAGES Kiongozi wa upinzani Gabon, Jean Ping, ametaka watu wasishirikiane na Ali Bongo kama kiongozi wa taifa baada ya uchaguzi wa Agosti uliokumbwa na mzozo. Kiongozi aliyepo sasa Bongo, alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo, lakini Ping anasisitiza kuwa yeye ndiye aliyeshinda. Upinzani unasema watu kadhaa waliuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi. Image copyright AFP Image caption Jean Ping Jean Ping ametia saini taarifa yake kama 'rais mteule' - wadhifa usiotambuliwa, na tume ya uchaguzi nchini. Kiongozi huyo wa upinzani ameshutumu alichokitaja kuwa mapinduzi ya kijeshi katika uchaguzi dhidi yake. Anataka raia wote wa Gabon wanaompinga rais Ali Bongo wajumuike na kushirikiana katika kumtenga kimataifa. Bwana Ping ametaka pia Bongo aidhinishiwe vikwazo na viongozi wengine kadhaa akiwemo mkuu wa mahakama ya katiba iliyopinga malalmiko aliyowasilisha kupinga uchaguzi huo. Lakini hatakama kuna wasiwasi wa kimataifa kuhusu...

Donald Trump. Mkanda watolewa wakati mbaya

MTEULE THE BEST Trump aliomba radhi Jumamosi (08.10.2016) kwa kutumia lugha hiyo chafu kuhusu kuwatomasa na kuwabusu wanawake katika mkanda wa video wa mwaka 2005.Kutolewa kwa mkanda huo kumeitibuwa kampeni yake na kusababisha kulaaniwa na wanachama wenzake kutoka chama chake mwenyewe cha kisiasa. Trump amesema katika taarifa ya video iliowekwa kwenye mtandao wa Twitter "Nimefanya mambo ninayoyajutia.Mtu yoyote anayenifahamu anajuwa kwamba maneno haya hayamaanishi mim ni mtu wa aina gani. Nimesema nilikuwa sio sahihi na naomba radhi." Wanachama wenzake wa chama cha Republikan wamelaani lugha aliyoitumia mgombea huyo.Spika wa Baraza la Wawakilishi Paul Ryan afisa mwandamizi wa chama hicho amesema "amechafuliwa " na matamshi hayo na amefuta tukio la kampeni lililokuwa lifanyike Wisconsin pamoja na Trump hapo Jumamosi. Wanachama wenzake wamuacha mkono Spika wa Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani Paul Ryan. Reince Preibus mwenyekiti wa Kam...

Trump aomba radhi kwa kuwatusi wanawake

MTEULE THE BEST Mgombea urais wa chama cha Republican Marekani, Donald Trump, ameomba msamaha kwa matamshi machafu aliyotoa kuhusu wanawake katika kanda ya video iliyozuka ya miaka 11 iliopita. Image copyr Mgombea urais wa chama cha Republican Marekani, Donald Trump, ameomba msamaha kwa matamshi machafu aliyotoa kuhusu wanawake katika kanda ya video iliyozuka ya miaka 11 iliopita. Katika kanda hiyo, Trump anasikika akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake sehemu zao za siri na kujaribi kushiriki ngono nao, anasema: 'unaweza kufanya chochote unapokuwa nyota'. Maafisa wakuu wa chama cha Republican wameshutumu vikali matamshi yake akiwemo spika wa bunge, Paul Ryan, aliyesema amechafuzwa roho na matamshi hayo. Mhariri wa BBC wa eneo la Amerika kaskazini anasema hiki ni kiwango cha mzozo katika azma ya Trump kuwania urais wa Marekani Katika kanda iliyorekodiwa Trump aliomba radhi kwa kuonekana akisoma , na ameahidi kuwa mwanamume bora zaidi lakini amemshutumu Bill Clinto...

KENYA:Shutuma zamuandama Chris Brown baada ya kutua

MTEULE THE BEST Muimbaji mashuhuri wa Marekani mtindo wa Hip Hop Chris Brown, yupo Kenya kwa tamasha la muziki mjini Mombasa eneo la pwani. Lakini tukio ambalo halikunukuliwa kwenye kamera limegubika vyombo vya habari nchini. Shabiki mmoja mwanamke anatuhumu kuwa Chris Brown ameivunja simu yake alipojaribu kupiga picha 'selfie' alipowasili katika uwanja wa ndege Mombasa. Kwa mujibu wa gazeti mmoja nchini "Daily Nation,'' mwanamke huyo anasema CB alimpokonya simu kutoka nyuma alipojitayarisha kuipiga picha hiyo na kuirusha chini. Taarifa hiyo inaongeza kuwa simu ya msichana huyo aina ya iPhone 6 iliyomgharimu takriban dola 900, haikuvunjika lakini kizuia kioo na kifunikio cha simu viliharibiwa. Shabiki huyo aliyesema amenunua tiketi kuhudhuria tamasha hilo, ameghadhabishwa na ameamua kutohudhuria tamasha hilo. Tuhuma zake zimesababisha gumzo kuu katika mtandao wa Twitter kupitia #DeportChrisBrown ambapo Wakenya wanajadili iwapo muimbaji huyo nyot...

Obama atangaza hali ya hatari Florida kutokana na kimbunga Hurricane Matthew

MTEULE THE BEST Image caption Obama ameviagiza vikosi vya uokoaji kuwa tiyari wakati wowote Rais wa Marekani Barrack Obama ametangaza hali ya hatari katika mji wa Florida baada ya picha za Satellite kuonyesha kimbunga Hurricane Matthew kinaelekea eneo hilo. Vikosi vya uokoaji navyo vimejiandaa kutoa msaada pale inapobidi. Kwasasa kimbunga Matthew kimesababisha kasi ya upepo kwenda kwa kilomita 220 kwa saa moja. Image caption Kimbunga Hurricane Matthew Mamilioni ya watu katika majimbo manne nchini Marekani wamenza kuhama makazi yao hususani aeneo ya mwambao wa pwani ili kuepuka kukumbwa naathari za moja kwa moja za kimbunga hicho.

Brazil: Rais Lula kuchunguzwa kwa tuhuma za ufisadi

MTEULE THE BEST Image caption Lula ameongoza Brazili kuanzia 2003 mpaka 2011 Mahakama kuu nchini Brazil imesema kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Luiz Inácio Lula da Silva atachunguzwa ili kuthibitisha kama kweli alihusika katika kashfa ya ufisadi kwenye kampuni kubwa ya mafuta nchini humo Petrobras. Waendesha mashitaka nchini humo wamesema kuwa Lula alikuwa muhimili mkubwa katika utekelezwaji wa rushwa hiyo. Lula amekana kuhusika na kusema kuwa hizo ni mbinu za kisiasa za kumzuia kuwania urais mwaka 2018.