MTEULE THE BEST Wengi tunajua kuwa alikuwa mhehe, ila leo nawaletea makala hii yenye kuchokoza mjadala juu ya Asili ya Chief Mkwawa. …………………………………… Mtwa Mkwawa hakuwa Mhehe na wala hakuwa mtoto wa Mnyigumba (kama historia iliyoandikwa na Wajerumani na inapotosha); bali Mkwawa alikuwa ni mtoto wa dada yake Mnyigumba ambaye aliolewa na Mtemi wa Waluguru. Hivyo Mkwawa alikuwa Mluguru kwa asili. Akiwa mdogo alikwenda kumtembelea mjomba wake (Mnyigumba) na kutokana na ushujaa wake, Mkwawa alishiriki kupiga vita vikali dhidi ya Wangoni pale Makambako. Mnyigumba akampenda Mkwawa kuliko watoto wake, na ndio chanzo cha kupewa urithi pamoja na mtoto wa Mnyigumba aliyeitwa Muhenga. Ndio maana Muhenga (mtoto orijino wa Munyigumba), akawa na bifu kali na Mkwawa na bifu hilo halikuisha hadi Muhenga alipofariki! Sherehe za kuapishwa Mtwa Mkwawa zilifanyika Dodoma eneo la Mpwapwa. Sherehe hizo zilihudhuriwa na wajomba zake—Mtemi Mazengo, Kimweri, Lugulu na Mirambo. Inasemekana ...