MTEULE THE BEST
Uingereza imepandisha kiwango cha kitisho cha mashambulizi ya kigaidi, ikiwa na maana kwamba shambulio jingine linaweza kutokea wakati wowote.
Kundi linalojiita "Dola la Kiislamu" limesema linahusika na shambulio hilo ambalo watu 29 wamejeruhiwa katika kituo cha treni kilichokuwa na watu wengi cha chini ya ardhi mjini London.
Polisi ya Uingereza imeanza kazi ya kumtafuta mtu aliyehusika na shambulio hilo jana kufuatia shambulio la kigaidi katika kituo cha treni mjini London. Kitu ambacho kilifichwa ndani ya ndoo ya plastiki pamoja na mfuko wa kununulia vitu unaotumika kwa kuwekwa katika friji uliripuka ndani ya behewa la treni lililojaa watu , na kuwajeruhi 29, wengi wao kwa kuungua.
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May
"Bila shaka, hiki kilikuwa kitu ambacho kilikusudiwa kusababisha madhara makubwa," waziri mkuu Theresa May alisema baada ya kuitisha mkutano wa kamati ya serikali ya kuchukua hatua za dharura inayojulikana kama COBRA.
Baadaye jana, May alisema kiwango cha hatari kwa nchi hiyo kimepandishwa kutoka hali mbaya na kwenda juu zaidi hadi hali mbaya sana, ambayo ina maana shambulio linatarajiwa wakati wowote.
"Umma utashuhudia polisi wengi zaidi katika mfumo wa usafiri na katika mitaa yetu wakitoa ulinzi wa ziada ," May amesema.
"Hii ni hatua sahihi na inayoeleweka ambayo itatoa uhakikisho wa ziada na ulinzi wakati mchakato wa uchunguzi ukiendelea."
Kamishna msaidizi wa polisi mjini London Mark Rowley akizungumza na waandishi habari kuhusu shambulio mjini humo
Kundi linalojiita "Dola la Kiislamu"
Kundi linalojiita Dola la Kiislamu limedai kundi linalojihusisha na kundi hilo linahusika na shambulio hilo, kwa mujibu wa kitengo cha propaganda cha kundi hilo cha Amaq. Ofisa anayehusika na kupambana na ugaidi nchini Uingereza amesema kundi la IS mara nyingi hudai kuhusika na mashambulio ambayo hayajahusika kabisa na kundi hilo na kwamba maafisa wanatafuta washukiwa na vitu vinavyoweza kusababisha kupatikana kwao.
Watu walioshuhudia wamesema kwamba majeraha yaliyasabishwa na mripuko wenyewe, wakati kwa wengine yalisababishwa na mkanyagano uliofuatia wakati abiria wa treni wakijaribu kuharakisha kutoka nje ya kituo hicho ambacho kwa kawaida kinatumiwa na watu wachache.
Uchunguzi umeanza kubaini utambulisho wa mshambuliaji
Wengine wanaeleza kwamba "mtafaruku ulitokea" wakati mamia ya watu wakijaribu kukimbia moto.
"Nilikandamizwa katika ngazi. Watu walikuwa wakiniangukia , watu walizimia, wakilia, kulikuwa na watoto wadogo waking'ang'ania mgongoni mwangu," Ryan Barnett mwenye umri wa miaka 25 aliliambia shirika la habari la The Associated Press.
Polisi ya Uingereza imesema mamia ya wapepelezi wanafanya mahojiano ya dharura kutaka kujua utambulisho wa mshambuliaji na wanasaidiwa na kitengo cha ujasusi
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni