Kimbunga Irma chapata nguvu kinapoelekea Florida

MTEULE THE BEST
Upepo mkali wa kimbunga Irma kimeanza kushuhudiwa FloridaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUpepo mkali wa kimbunga Irma kimeanza kushuhudiwa Florida
Nguvu ya upepo mkali unaondamana na kimbunga, kimeanza kugonga visiwa kadhaa kusini mwa jimbo la Florida nchini Marekani, huku kimbunga kikiacha uharibifu mkubwa katika visiwa vilivyoko kwenye bahari ya Atlantic huko Caribbean, kuelekea Marekani.
Kimbunga Irma, kinatarajiwa kugonga maeneo hayo, baadaye leo Jumapili.
Viwango vya maji tayari vimeanza kuogezeka katika maeneo ya pwani ya Florida, eneo ambalo linatarajia kimbunga kikubwa kuwasili.
Taharuki na hatma ya baadaye ya mji wa Tampa, ambao unakabiliana ana kwa ana na njia inakopitia kimbunga hicho, haijulikani.
Ramani ya mwendo wa Kimbunga Irma
Image captionRamani ya mwendo wa Kimbunga Irma
Tampa inasemekana kuwa ni mji ulioko katika mazingira magumu zaidi nchini Marekani, hasa kuhusiana na hatari ya kugongwa mara kwa mara na vimbunga.
Zaidi ya watu milioni 6 huko Florida wanaondolewa majumbani mwao- robo tatu ya idadi nzima ya watu wa jimbo hilo.
Wakuu katika jimbo hilo wametangaza hali ya tahadhari ya kutotoka nje, katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo, ukiwemo mji wa Miami.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU