MTEULE THE BEST
Klabu ya Celtic ilipokea kichapo kikubwa zaidi nyumbani huku Neymar akiiongoza PSG katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Neymar ambaye ndio mchezaji ghali duniani aliifungia timu yake mpya na kusaidia kupatikana kwa bao la pili ambalo lilifungwa na Kylian Mbappe.
Edison Cavani alifunga bao la tatu kwa njia ya penalti na hivyobasi kuwahkikishia wageni hao uongozi kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza.
Bao alilojifunga Mikael Lustigs lilifuatiwa na bao la pili la Cavani ambalo lilifungwa kupitia kichwa kizuri.
Celtic imekuwa mwenyeji wa timu kubwa za bara Ulaya katika kombe hilo katika miaka ya hivi karibuni, lakini hata wale waliokuwepo katika zama za klabu hiyo hawajawahi kushuhudia kipigo kama hicho cha 5-0.
Kasi yao, mafikira na mchezo wao ulikuwa wa kiwango cha hali ya juu.
Maoni