MTEULE THE BEST
Rais wa Tunisia ametanga kuwa wanawake sasa wako huru kuolewa na wanaume wasio waislamu, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP
Tangazo hilo linakuja mwezi mmoja baada ya Rais Beji Caid Essebsi, kutoa wito kwa serikali kuondoa marufuku hiyo ya mwaka 1973.
Hadi sasa mwanamume ambaye si muislamu anayetaka kumuoa mwanamke wa Tunisia, alihitaji kubadili dini na kuwa muislamu na kutoa cheti cha kuonyesha kuwa amefanya hivyo.
- Klabu yafungwa kwa kucheza muziki wa 'Adhan' Tunisia
- DJ aliyecheza ''Adhan'' katika klabu kufungwa jela
- Merkel ataka kufahamu zaidi kuhusu mshambulizi wa Berlin
Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Tunisia yamekuwa yakifanya kampeni ya kutaka kuondolewa marufuku hiyo wakisema kuwa inakiuka haki za binadamu za kumchagua mke au mume.
Tunisia inaonekana kuwa iliyopiga hatua mbele ya mataifa mengine katika masuala ya haki za wanawake, lakini bado kuna ubaguzi katika masuala ya urithi
Maoni