David Luiz Barcelona watatoa ofa ya pauni milioni 130 kumnunua Coutinho, 25, wiki hii, na wana uhakika kuwa watampata mchezaji huyo wa Liverpool ambaye walikosa kumnunua msimu uliopita. (Sunday Mirror) Arsenal wana nia ya kumsaini beki wa Chelsea David Luiz, lakini ikiwa Chelsea hawataki kuumuuza mchezaji huyo wa miaka 30 kwa mahasimu wao basi mbrazil huyo ataelekea Juventus. (Sunday Express) West Ham, wana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Andre Schurrle, 27, kutoka Borussia Dortmund. (Bild huko German) Emre Can Bayern Munich na Manchester City wanaaminiwa kujiunga katika mbio za kumpata kiungo wa kati wa Liverpol na Ujerumani Emre Can, 23. (Tuttosport - in Italian) Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anasema hajui mipango ya mshambuliaji Alexis Sanchez kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. (Sunday Times) Ajenti wa Alexis Sanchez amezungumza na Manchester City kuwashawishi kumpa ofa ya mweze Januari mchezaji huyo ambaye anataka kuondoka Arsenal....