Spika wa Bunge la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema Demokrasia ya Wamarekani iko mashakani, rais anawaacha bila chaguo Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani Nancy Pelosi anasema bunge hilo litawasilisha mashtaka ya uchunguzi dhidi ya rais Donald Trump, kwa madai ya matumizi mabaya ya mamlaka yake. "Demokrasia yetu iko mashakani, rais anatuacha bila chaguo la kufanya," alisema kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa Democrat. Ameyasema hayo siku moja baada ya kamati ya masuala ya sheria ya bunge kuanza kuangalia mashitaka yanayoweza kuwasilishwa dhidi ya rais huyo kutoka chama cha Republican. Bwana Trump aliwaambia Wademokrats kama watataka kumshitaki basi waharakishe. Alituma ujumbe wa Twitter muda mfupi kabla ya kauli za Bi Pelosi : " Kama mtanichunguza, mfanye sasa hivi, haraka, ili tuwe na kesi ya haki katika Seneti, ili nchi iweze kuendelea na shughuli za kawaida'': Mbunge wa Congres jimbo la California, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari A...