MTEULE THE BEST
MAKADIRIO YA BAJETI KENYA, TANZANIA, UGANDA
KENYA
Nchini kenya waziri wa fedha Henry
Rotich leo amewasilisha bungeni bajeti ya makadirio ya matumizi ya pesa
za serikali katika kipindi cha mwaka 2016-2017.
Bajeti hiyo ya
jumla ya shilingi trilioni 2.26 inatarajiwa kufadhiliwa kupitia
ukusanyaji wa ushuru na mikopo kutoka kwa washirika wa kimaendeleo.
Serikali inalenga kukopa shilingi bilioni 778 hatua ambayo itaongeza
deni la kenya ambalo kufikia sasa ni shilingi trilioni 3.32.Matumizi zaidi itaelekezwa kwa ujenzi wa miundo mbinu ikiwa ni pamoja ujenzi wa reli ya kisasa, kuimarisha usalama, huduma za afya na pia kuziwezesha serikali za majimbo.
Kama ilivyo ada bajeti inaposomwa kuna wale wa wanaofaidi na wale wanaopoteza. Gesi ya kupikia na chakula cha mifugo umeondolewa ushuru, Huku ushuru wa petroli na mafuta taa ukiongezwa. Bidhaa za mafuta ya urembo zikiwekewa ushuru wa asilimia kumi kwa mara ya kwanza.
Waziri ametenga shilingi bilioni 4.3 kwa huduma za bure za wanawake wajawazito kujifungua,milioni 19.7 kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 na shilingi milioni 7.9 kwa watoto mayatima.
TANZANIA
Waziri wa Fedha nchini Tanzania Phillip Mpango alisema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 18.46 zitatokana na jumla ya mapato ya ndani.
Kiwango hicho kimezidi shilingi trilioni 3.64 za bajeti iliyopita ambayo ililenga kukusanya shilingi trilioni 4.82.
Shilingi trilioni 17.72 zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku trilioni 11.82 sawa na asilimia 40 ya bajeti nzima, zikitengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Bwana Mpango alisema washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia shilingi trilioni 3.6, ikiwa ni ongezeko la shilingi trilioni 1.7 ikilinganishwa na shilingi trilioni 1.88 zilizokuwa zinategemewa kwenye bajeti iliyopita.
UGANDA
Bajei kubwa mwaka huu nchini Uganda imeelekezwa kwa wizara ya kazi na uchukuzi ambayo ilipewa dola blioni 1.1 huku wizara ya ulinzia ikipewa dola milioni 435. Wizara ya afya imepata dola milioni 525.
Wizara ya nishati na maendeleo ya madini ilipata dola milioni 695 huku Wizara ya kilimo ambayo ndiyo muhimu nchi Uganda ikiwa dola milioni 522.
Maoni