Vyama vya upinzani nchini Tanzania vimelaani hatua ya polisi nchini humo kupiga marufuku mikutano ya hadhara
MTEULE THE BEST
Vyama vya upinzani nchini Tanzania vimelaani hatua ya polisi nchini humo kupiga marufuku mikutano ya hadhara.
Jana polisi waliwatawanya wafuasi wa vyama vya upinzani mjini Kahama, Magharibi Kaskazini mwa Tanzania, ambapo walikuwa wamekusanyika muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara uliokuwa umeandaliwa na chama cha ChademaHata hivyo polisi wamesema kutokana na sababu za kiusalama, hawataruhusu mikutano hiyo iendelee kufanyika.
Wameongeza pia kwamba mikutano hiyo ilikuwa inalenga kuwashawishi wananchi kuvunja sheria.
"Hizi ni siasa za kibabe na kidikteta ambazo Rais Magufuli ameanza kuzionyesha kwanza kwa kuzuia bunge lisionekane moja kwa moja na sasa wanazuia mikutano ya hadhara" amenukuliwa bw Mbowe na gazeti moja la kila siku nchini Tanzania.
Maoni