RAIS WA SOMALIA AZURU KAMBI YA WAKIMBIZI DAADAB
Mashariki mwa Kenya.
Daadab ni miongoni mwa kambi za wakimbizi ambazo zina idadi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani.- Kenya: Wakimbizi Daadab kurejeshwa kwao Novemba
- Wakimbizi wa Somalia warejeshwa kwao
- Tahadhari Kenya wakati wa Ramadhani
Mwandishi wa BBC Bashkash Jugsoday aliyeko Garissa nchini Kenya anaelezea alivyopokewa kwa furaha na bashasha huko Garissa siku ya mwanzo wa mfungo wa Ramadhan.
Kambi hiyo ilizinduliwa yapata miaka ishirini na tano iliyopita ilikuwapa uhifadhi raia wa Somalia ambao walikuwa wakitoroka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Hata hivyo, hivi karibuni, serikali ya Kenya imesema wakati umefika kwa kambi hiyo kufungwa.
Kenya inalalamikia utovu wa usalama kufuatia habari za kijasusi zilizodai kuwa wanamgambo wa Al Shabaab wanatumia kambi hiyo ya wakimbizi kubwa zaidi nchini Kenya kupanga mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.
Awali mpango sawa na huu wa kuwarejesha kwao wakimbizi haukufaulu huku serikali ya Kenya ikilaumu washirika wake yaani Serikali ya Somalia naShirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia maswala ya wakimbizi,UNHCR kwa utepetevu.
Kenya inasisitiza kuwa ina haki ya kimsingi ya kuwalinda raia wake mbali na kuwa na jukumu la kuwapa hifadhi wakimbizi ambao sasa wamanza kuhujumu usalama wake.
Aidha Serikali ya Kenya inasema kuwa mazingira yameharibiwa sana katika eneo hilo lenye ukame.
Juma lililopita Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya bwana Joseph Nkaisserry alikariri kauli ya serikali yake kuwa hakutakuwa na mazungumzo zaidi kuhusiana na hilo.
Waziri huyo aliambia BBC kuwa serikali kwa ushirikiano na serikali ya Somalia na kitengo kinachoshughulikia maswala ya wakimbizi cha Umoja wa Mataifa UNHCR zitahakikisha uhamisho huo inafanyika kwa njia nzuri.
Kenya tayari imetenga takriban dola milioni kumi kufanikisha shughuli hiyo ambayo inasema kuwa inalenga kuihakikishia usalama wake kufuatia msururu wa mashambulizi ya kigaidi yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la al Shabaab.
Maoni