Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MATENDO MAOVU YA NDOA

MTEULE THE BEST

MTEULE THE BEST  TUMSIFU YESU KRISTO!!!

MADA YA LEO:-    

             MATENDO MAOVU YA NDOA


 SOMA WALAWI 18:1-30

MWENYEZI-MUNGU alimwambia MOSE "waambie watu wa Israel hivi: 

Mimi ndimi MWENYEZI-MUNGU MUNGU WENU

Kamwe msifanye kama walivyofanya watu wa misri ambako mlikaa; wala msifanye kama wafanyavyo watu wa nchi ya kanaani ambako  nawapeleka 

kamwe msifuate mitindo yao  ninyimtafata maagizo yangu na kuyashika masharti yangu  mimi ndimi MWENYEZI-MUNGU MUNGU WENU 

''Mtu yeyote wa israel haruhusiwi kumkaribia mtu wajaa yake wa karibu ili kulala naye mimi ndimi MWENYEZI-MUNGU MUNGU WENU  

kamwe usimvunjie heshima baba yako kwa kulala na mama yako aliyekuzaa usimwaibishe yeye ni mama yako 

kamwe usimvunjie heshima baba yako kwa kulala na moja ya wake zake hao ni mama zako 

kamwe usilale na dada yako awe dada yako  halisi au dada wa kambo 

kamwe usilale na mjukuu wako ,mtoto wa mwanao  au binti yako maana sehemu zao za siri ni kama zako mwenyewe 

kamwe usilale na msichana aliyezaliwa na mama yako wa kambo aliyeolewa na baba yako msichana huyo ni dada yako 

kamwe usilale na shangazi yako kwani huyo ni dada wa baba yako

kamwe usilale na dada ya mama yako  kwani huyo nimama yako mkubwa au mdogo 

kamwe usilale na mke wa baba yako mkubwa au mdogo,huyo nimama yako 

kamwe usilale na mke wa mwanao , huyo ni mkewe mwanao kamwe usilale naye

kamwe usilale na mke wa ndugu yako huyo ni shemeji yako 

ukilala na mwanamke basi kamwe usilale naye na binti yake wala wajukuu zake hao ni ndugu kuwachanganya ni kufanya uovu 

kamwe usimwoe dada wa mkeo wakati mke wako yungali hai ; hiyo itasababisha ushindani

kamwe usilale na mwana mke awapo mwezini 

kamwe usilale na mke wa jirani yako na hivyo kujitia mwenyewe najisi naye 

kamwe usimtoe mtoto wako yeyote kuwa sadaka  kwa mungu-moleki maana kufanya hivyo hutalikufuru jina langu mimi MUNGU wako mimi ndimi  MWENYEZI-MUNGU MUNGU WENU  

kamwe  usilale na mwanaume mwenzio kana-kwamba mwanamke hilo ni chukizo 

kamwe usilale na mnyama ili ujitie najisi mwanaume au mwanamke yeyote kamwe asifanye hivyo ;kufanya hivyo ni upotevu

 

Msijitie najisi kwa kufanya hayo mambo kwani kwasababu ya mambo hayo nawafukuza mataifa yaliyo mbele yenu kwa vile hufanya hayo na kujitia najisi

nchi yao ilitiwa najisi nami nikaiadhibu nayo ikawakataa wakazi wake 

lakini nyinyi na wageni wanao kaa kati yenu ni lazima kuyashika masharti  na maagizo yangu  na wala msifanye machukizo hayo 

machukizo hayo walifanya watu waliokaa katika nchi ya kanaani kabla yenu ,nao wakaitia nchi najisi 

basi nyinyi msifanye mambo hayo la sivyo nchi itawatapika kama ilivyo watapika taifa lililokuwa kabla yenu 

watu wote watakaofanya mambo hayo ya kuchukiza ni lazima watengwe mbali na watu wao 

kwahiyo sikien kikamilifu yote ninayo waagiza ;msifate mazoea yeyote ya kuchukiza yaliyofanywa na wale walioishi nchini kabla yenu msije mkajitia najisi kwayo 

mimi ndimi

MWENYEZI-MUNGU MUNGU WENU  

NENO LA BWANA

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...