MTEULE THE BEST
Rais wa Marekani
Barack Obama
ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa chama
cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu
nchini Marekani.
Amechukua hatua hiyo muda mfupi baada ya kukutana
na seneta wa Vermont Bernie Sanders ambaye amekuwa akikabiliana na Bi
Clinton katika kinyangāanyiro cha kumchagua mgombea wa chama hicho.Akizungumza kwenye video ambayo imepakiwa kwenye Twitter na Bi Clinton, Bw Obama amesema mgombea huyo ndiye aliyewahi kuhitimu zaidi kuwa rais wa Marekani.
āNiko pamoja naye, nina msisimko na nasubiri sana kutoka huko nje na kufanya kampeni na Hillary,ā amesema Obama.
Bw Sanders naye amesema yuko tayari kufanya kazi na mpinzani wake, Bi Clinton, kumshinda mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika uchaguzi mkuu.
Hata hivyo hakujiondoa kinyangāanyironi. Alisema ataendelea kufanya kampeni yake na kwamba anatumai atakutana na Bi Clinton hivi karibuni.
Maoni