Mikutano na maandamano ni marufuku Tanzania

MTEULE THE BEST

Polisi nchini Tanzania wamepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia Jumanne wiki hii hadi hali ya usalama itakapotulia

Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari walinda usalama hao wamewataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi.
Taarifa hiyo imesema kuwa polisi hawatasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hilo.
Aidha maafisa hao wamewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi na badala yake kuwasihi waendelee kushirikiana katika kujenga Umoja wa taifa la Tanzania.
Polisi nchini Tanzania imeripoti kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya kisiasa vikitaka kufanya mikutano na maandamano .
Hata hivyo, maafisa hao kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya habari wamebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi

 mikakati ya chadema ya mikitano nchi nzima hakuna tena maana

Mikutano na maandamano ni marufuku Tanzania unazungumzia hili iwe kijana m

hata wakubwa zetu 

je nisawa ama si sawa




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU