Nyota wa Leicester City Jamie Vardy amesalia kimya kuhusu uwezekano wake wa kuhamia klabu ya Arsenal.
MTEULE THE BEST
Nyota wa Leicester City Jamie Vardy amesalia kimya kuhusu uwezekano wake wa kuhamia klabu ya Arsenal.
Mshambuliaji
huyo wa England mwenye umri wa miaka 29 alipangiwa kuamua iwapo
atasalia na Leicester au atajiunga na Gunners kabla yake kusafiri
kuelekea Ufaranca kushiriki michuano ya Euro 2016 itakayong’oa nanga
Ufaranza Jumatatu.Lakini ameabiri ndege pamoja na wenzake wa timu ya taifa ya England bila kufahamisha Arsenal uamuzi wake.
Vardy bado anatarajiwa kufanya uamuzi kuhusu ofa ya Arsenal ya kumuahidi ujira wa £120,000 kila wiki baadaye leo Jumatatu.
Arsenal wanadaiwa kuahidi kulipa £20m kumnunua Vardy, bei ambayo itamuweka huru kutoka kwa mkataba wake na Leicester.
Nyota huyo wa zamani wa Fleetwood Town alitia saini mkataba wa miaka mitatu wa kulipwa hadi £80,000 kila wiki Leicester Februari.
Vardy alijiunga na Leicester akitokea Fleetwood kwa £1m mwaka 2012.
Aliwafungia mabao 24 na kuwasaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita.
Maoni