TEC YARUDISHA $5 milion

MTEULE THE BEST

Tume ya uchaguzi nchini Tanzania TEC imerudisha takriba
n dola milioni 5 kwa serikali baada ya kutotumika katika uchaguzi wa mwaka jana.
Mwenyekiti wa tume hiyo Damian Lubuva alimkabidhi rais John Pombe Magufuli fedha hizo.
Bw Lubuva amesisitiza kuwa uchaguzi uliendeshwa kwa njia nzuri bila fedha hizo.
''Bw Rais ,tulikuwa wagumu lakini tulifanikiwa kufanya kazi zetu vzuri.Kwa hivyo hizi zilizosalia hazimaanishi kwamba kazi yetu haikuafikia mahitaji yake''.
Rais Magufuli ameitaja hatua hiyo kuwa ya kizalendo.
''Mungezificha fedha hizi na kusema kwamba zilitumika zote ,ama hata kusema hazikutosha na hakuna mtu angewauliza''.
Rais Magufuli ameamrisha fedha hizo kutumika kujenga afisi za tume hiyo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU