MTEULE THE BEST
Rais Barrack Obama wa Marekani
amesema kwenye mahojiano na runinga moja kuwa anatarajia chama chake cha
Democratic kitaungana zaidi katika kipindi cha wiki chache zijazo.
Matamshi
yake yamejiri baada ya Hillary Clinton kushinda uteuzi wa chama hicho
kuwania kiti cha urais, baada ya kushinda idadi ya wajumbe katika uteuzi
wa mashinani.Obama ametaja Bi Clinton kama 'Kiranja shupavu' na wakati huo huo kumpongeza mpinzani wake Bernie Sanders kwa kuendesha kampeini na kujadili masuala muhimu ya kijamii.
Sanders ambaye hajakubali kushindwa, anatarajiwa kukutana na rais Obama baadaye hii leo.
![]() |
SANDERS & HILLARY |
Maoni